Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) – ABNA – Darsa ya Qur’ani Tukufu imefanyika leo, Alhamisi, tarehe 1 Oktoba 2026, kwa wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa Mbezi Beach, Dar es Salaam, Tanzania.
Darsa hiyo imeongozwa na Sheikh Muhammad Jafar, ambapo wanafunzi wamepata fursa ya kujifunza na kuongeza uelewa wao kuhusu namna sahihi ya kusoma Qur’ani Tukufu.

Katika somo hilo, wanafunzi wamefundishwa kanuni mbalimbali za usomaji sahihi wa Qur’ani Tukufu, pamoja na hukumu zinazohusiana na usomaji wa Qur’ani. Aidha, wamejifunza kuhusu umuhimu wa kufahamu maana ya Aya za Qur’ani na kuzitafakari kwa kina.
Vilevile, darsa hiyo imejikita katika kuwahimiza wanafunzi kufanya Tadaburi katika Aya za Qur’ani Tukufu, kwa lengo la kutambua ujumbe, mafunzo na mwongozo unaopatikana ndani ya Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.

Darsa kama hii ni sehemu ya programu za elimu ya Qur’ani na malezi ya kidini zinazofanyika katika vituo vya Jamiat Al-Mustafa, kwa ajili ya kuwajengea wanafunzi uwezo wa kusoma Qur’ani kwa usahihi na kuielewa pamoja na kutekeleza mafundisho yake katika maisha ya kila siku.



Maoni yako